Zulu Unity Is Power


wanajiuliza na hawajawahi pata majibu sahihi hususan wale ambao wako kwenye lindi la mapenzi.Baadhi ya wasanii kama vile Bahati Musyoka msanii wa nyimbo za injili 
ameweza kuangazia swala hili katika wimbo wake na kusadiki kuwa mapenzi yalianzia kwenye shamba  la edeni, mie sijui kama ni kweli.
Wanafunzi wengi katika vyuo vikuu nchini wanajitia  kwenye uhusiano bila kujua hatima yake.Kila mmoja anatamani kuwa na  mpenzi   kwa sababu wana uhuru kupindukia.Kutokana na uchunguzi nilioufanya, asilimia kubwa ya mahusiano   ya kimapenzi vyuoni hayadumu.Uchunguzi wangu ulidhihirisha kuwa wanafunzi wengi si waaminifu na mara nyingi huwa na “michepuko”.Mwanaume anaweza kuwa na mchumba  zaidi ya mmoja  jambo ambalo si tofauti kwa wasichana.Kusudi la washichana au wavulana kuchepuka au kusaliti uhusiano ni upi?Uchunguzi ulidhihirisha kuwa wengi wao hutaka kukidhiwa mahitaji ya kifedha bila kuzingatia kuwa wanaowategemea ni wanafunzi kama wao.
Swala la udananyifu na kutoaminiana kwenye uhusiano limekuwa donda dugu  chuoni humo.Baadhi ya matukio ya kusikitisha yameweza kutokea ambapo wanafuzi wa kiume wameweza kupigana makonde ,huku wengine wakiwarusha wenzao kutoka ghorofa za hosteli za wanafunzi.Tukio la hivi karibuni likiripotiwa hosteli nambari nne(HB4).
Kipindi cha utamu na ula roda na mchumba huisha pale tu “mali” mpya inapoingia sokoni.Hawa ni makomredi wapya,ambao ni mwanzo wanajiunga na chuo kikuu-Almaarufu “Fresher”.Wanafunzi hawa wapya hutekwa na makomredi wakongwe na kupelekwa katika “mafunzo” maalum na “kuchanuliwa”.”Walimu” hawa wana bidii kiasi cha kuwa na chama-almaarufu “mafisi Sacco” .
Kizungumkuti ni kwa wale walojitia mapenzini na kibahati mbaya jahazi likawaendea mrama.Je,watajikaza kuujenga ama kuuangamiza zaidi uhusiano wao? Ila hilo halinihusu.Kama umeyavulia nguo,huna budi kuyaoga.

Comments